Shirikisho la Vyama vya Madereva nchini Tanzania (TDF) limemchagua aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito wa shirikisho hilo, Abdalah Lubala kuwa rais wa Shirikisho kwa muda wa miaka minne,

Uchaguzi huo umefanyika hii leo Jijini Dar es salaam ambapo mpinzani wa Lubala, Wito Zabron Mbwilo alijitoa katika uchaguzi huo na kumfanya Rais Lubala kupita bila kupingwa katika nafasi hiyo,

Nafasi ya Makamu wa Rais imechukuliwa na Mwinyi Mangara aliyepata kura 40, dhidi ya mpinzani wake Elikana Gidion aliyepata kura 3 na kumfanya kuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo la Madereva nchini Tanzania.

Aidha, katika mkutano huo, pia shirikisho hilo limeweza kuchagua kamati mbalimbali za uongozi zitakazo shirikiana na uongozi wa ngazi ya juu katika kutoa miongozo ya kiutendaji ndani ya shirikisho hilo.

Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa, Rais Lubala amewaahidi wajumbe wa kamati na wanachama wa shirikisho hilo kutoa ushirikiano wa hali ya juu katika kutetea maslahi ya Madereva nchini,

“Kwanza nawashukuruni sana wajumbe kwa kunaiamini na kunichagua kuongoza Shirikisho la Vyama vya Madereva Tanzania (TDF) kwakweli niwahakikishie kwamba nitafanya kazi kwa maslahi ya Madereva nchini na nitahakikisha kuwa napunguza kero ambazo zimekuwa zikiwakumba  Madereva,” amesema Rais Lubala

Canelo ampiga Golovkin, matokeo yazua utata tena
Video: Vyama vya Madereva nchini vyaunda SHIRIKISHO (TDF)