Mtayarishaji wa muziki nchini, Shirko ambaye kwa muda mrefu amekuwa akisikika kwenye nyimbo zenye asili ya Kitanzania, amesuka mtindo wake mpya wa muziki kwa mikono yake.

Shirko ameupima muziki wa Nigeria ambao umekuwa ukiigwa na na kupendwa na Watanzania wengi huku muziki wa Bongo Flava ukigeuka kuwa Naija Flava kwa asilimia kubwa na ameamua kuja na mkombozi ambaye atakuwa mbadala.

Akiongea na Jabir Saleh, mtangazaji wa Ladha 3600 ya E-FM, Shirko amesema kuwa ameunda aina mpya ya muziki aliubatiza jina la ‘Dance Bongo Flava.

“Kuliko muziki wa Bongo Flava uhamie kwenye Naija moja kwa moja watu wakopi na ku-paste kurudisha huku wakiimba Kiswahili, nikaona kwamba tunauwezo wa kuchukua labda temple yao na vitu ambavyo vingeweza kuendana na wakati, tuchanganye na flava zetu. Of course Mungu akanijalia nikapata kitu kinaitwa Dance Bongo Flava,” Shirko aliiambia Ladha 3600 ya E-Fm.

Katika hatua nyingine, Shirko amesema kuwa moyo wake na mapenzi yake zaidi yako kwenye muziki wa asili ambao amekuwa akiutumia kuunda hits kadhaa. Alisema kuwa mtindo huo ndio uliomfanya Diamond Platinumz kumpigia ‘salute’ kwenye muziki wenye vionjo vya asili.

Shirko alipata umaarufu na kutambulika zaidi baada ya kufanya kazi na Berry Black na Berry White akiwa kama mtayarishaji wa muziki wao na muimbaji pia. Hivi sasa amekuwa akipika nyimbo za ‘Mkubwa na Wanae’.

Kupanda Mabasi ya Mwendo kasi jijini Dar sasa ni kwa Kadi
Serikali Itaendelea Kufanyabiashara na Wachina