Naibu Waziri wa Sanaa, Habari, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza amewataka wasanii kuacha kutafuta kiki mitandoni na kufanya vitu ambavyo vitawaletea manufaa na kuweka heshima kwa jamii na kuacha kutumia nguvu nyingi kwenye vitu visivyo eleweka.
Shonza amesema hayo wakati alipohudhuria uzinduzi wa mpango wa mwigizaji mkongwe wa sinema za Kibongo, Yvone- Cherry Ngatikwa maarufu kama ‘Monalisa’ kwa kuinua vipaji vya filamu kwa wasichana uitwao Mona ACT uliofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar.
Aidha katika uzinduzi huo, ulishindanisha wasichana 500 na kupatikana wasichana 50 ambao walionesha umahiri mkubwa katika kuigiza. Shonza ameongeza kuwa msanii anatakiwa apate umaarufu mkubwa kupitia kazi zake anazo fanya. Aidha ameongeza kuwa mtu kama fey yeye hawezi kumuita msanii inabidi umaarufu uupatie kwenye kazi nasio kiki kila kukicha”.
Hata hivyo Shonza aliwasihi wasichana hao kutafuta umaarufu kupitia vipaji vya sanaa na kuachana na kiki zisizokuwa na maana.