Waziri wa Habari, Sanaa na Utamaduni Juliana Shonza amefunguka na kusema hawezi kujibizana na Diamond, zaidi tu amewataka wananchi watambue kuwa hakuna  aliye juu ya sheria.

Shonza amesema amesikia malalamiko ya  mwanamuziki huyo na amesema zipo taratibu za kufuata kama anaona hajatendewa haki.

Aidha Shonza amezungumza amesema

‘’Aliyewafungia wasanii si Shonza bali ni mamlaka na kama mlivyoona safari hii hadi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeingilia kati suala hilo, sasa mtu anaporusha tuhuma kumlaumu Shonza atakuwa hanitendei haki. Isitoshe ofisi zetu zipo wazi anayeona ameonewa afuate taratibu katika kudai haki yake si kulalamika pembeni amesema Waziri Shonza.

Pia Shonza amejibu tuhuma kuhusu wasanii hao kufungiwa nyimbo zao bila ya kuitwa na Basata amesema kuwa swali hilo wawaulize Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

Shonza amefunguka hayo baada ya msanii Diamond Platinumz kudai kuwa Waziri Shonza amekuwa akifanya maamuzi yake kwa kukurupuka akisahau kwamba viongozi hawana mchango wowote kwao na pia wamekuwa wakiziumiza familia zao.

‘’Hivi leo unanifungia nyimbo yangu niliyoitengeneza kwa mamilioni ya pesa unadhani nitazirudishaje, au unadhani watoto wangu Nillan, Tiffah  na Dylan watanunuliwa na nini Pampas? Ifike mahali viongozi wetu wavae vyetu na si kuona raha tu kutufungia wakati tumetaabika katika kuyajenga majina yetu hadi sasa tunajulikana’’ hayo amezungumza Diamond.

Aidha Diamond Platinumz amefunguka hayo kufuatia nyimbo 15 za wasanii zilizofungiwa huku zikiwemo zakwake mbili, ya Alleluyah na Wakawaka.

 

 

Dismas Ten awatolea uvivu mashabiki wa Yanga
Waandamanaji 47 wauawa wakimpinga Rais Kabila