Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Joseph Nyamhanga amezitaka shule binafsi nchini kuweka kiwango cha ada ambacho kitawezesha watanzania wengi kumudu.

Nyamhanga ameyasema hayo leo Januari 5, 2021 wakati akifungua mkutano wa pili wa Umoja wa walimu wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo.

Nyamhanga amesisitiza kwa sekta hizo binafsi kuifanya elimu kama huduma kwa watanzania na sio kuifanya kama biashara kwa kuweka kiwango kikubwa cha ada.

Katibu Mkuu huyo amesema shule binafsi zimesaidia kuleta ushindani na zimekuwa mfano wa jinsi ya kusimamia elimu kwa shule za serikali, ushindani ambao umesaidia kuzifanya  shule za serikali za msingi na sekondari kujifunza  usimamizi mzuri wa kutoa elimu.

Aidha, amewataka walimu kudhibiti wizi wa mitihani na kwamba isitokee kwa ngazi zote za elimu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TAPSHA, Rehema Ramote, ameametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa kuajiri walimu 8,000.

Kilo 4,880 za Sukari ya magendo zagawanywa kwenye taasisi
Benchi la ufundi Gwambina FC lapigwa chini