Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametangaza kulegeza masharti ya kudhibiti Ugonjwa wa Covid 19 kwa kufungua mipaka ya kimataifa, kuruhusu utalii kurejea, shule kufunguliwa, michezo kurejea pamoja na kufungua nyumba za ibada.

Rais Museveni amesema hayo wakati akitoa hotuba kupitia televisheni Septemba 20, 2020, ambapo wageni wanoingia nchini humo wanalazimika kufanya vipimo vya corona, saa 72 kabla ya kuwasili.

Hata hivyo wanafunzi wanaomaliza shule ya msingi, sekondari na taasisi za ufundi na biashara watafungua shule katikati ya mwezi Oktoba mwaka huu.

Aidha Rais Museveni, amesema madarasa mengine yatafunguliwa Januari mwakani.

Vile vile michezo ya nje imeruhusiwa kurejea, lakini haitakuwa na mashabiki ambapo wachezaji walikuwa katika msimu wa kujitenga wanapaswa kuwa wamepimwa saa 72 kabla ya michuano katika kila wiki mbili.

Makatazo mengine kama zuio la mikusanyiko ya umma na kutembea usiku kuanzia saa tatu hadi 12 asubuhi yataendelea nchini humo.

Mpaka hivi sasa maambukizi ya ugonjwa wa covid 19 ymefikia takribani watu 6,287, huku vifo vikifikia 63.

Son: Ninafuraha sana kufunga mabao manne
TFF: Karia ruhsa kugombea FIFA