Waalimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wamepongezwa kwa kazi nzuri ya kupata matokeo mazuri ya shule zao za msingi katika mtihani wa taifa wa mwaka jana.

Pongezi hizo zimetolewa na mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Sigisbert Rwezaula wakati wa hafla ya kupongeza shule kumi zilizofanya vizuri katika mitihani ya mwaka jana.

Hafla hiyo ilifanyika Mwadui wilayani Kishapu ikiambatana na utoaji vyeti kwa walimu wakuu, Rwezaula ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema kuwa hakuna muujiza wa kufanya vizuri bali ni waalimu kujituma.

”Najua kuna changamoto nyingi kwa walimu kama upungufu au ukosefu wa fedha lakini nawaomba tuvumilie na tukabiliane nazo, jambo kubwa ni kutoa elimu bora kwa wanafunzi wetu na hatimaye wafanye vizuri,” amesema Rwezaula.

Aidha, Rwezaula ametoa rai kwa waalimu wa shule hizo za msingi zilizopo katika Halmashauri hiyo kuwa na utamaduni wa kujiendeleza kimasomo ili kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Hata hivyo, katika Kikao hicho kilichofanyika Mwadui kilihusisha Maofisa Elimu Msingi, Waratibu Elimu Kata, Walimu Wakuu na badhi ya walimu wa shule mbalimbali za msingi zilizopo Wilaya ya Kishapu

Madaktari 470 wachangamkia fursa nchini Kenya
Niyonzima anena kuelekea pambano lao dhidi ya Azam FC