Katibu Mkuu chama cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo amesema katika matokeo ya mtihani mwaka huu karibu asilimia 80 hadi 90 ya wanafunzi wanaosoma katika shule zinazomilikiwa na chama wamepata ufaulu wa daraja la kwanza na la pili huku mwanafunzi mmoja tu akipata ufaulu wa daraja la nne.

Amebainisha hayo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa semina ya watumishi wa taasisi za elimu zinazomilikiwa na jumuiya ya wazazi ya chama hicho.

Chongolo amesema lengo la chama kuanzisha shule ni kuwezesha vijana wote kupata elimu bora.

Aidha, ametoa wito kwa jumuiya ya wazazi kuendelea kuwajengea uwezo viongozi wa shule ili heshima ya wakuu wa shule iendane na muda aliokaa katika shule.

Hata hivyo, amesisitiza kwa wakuu wa shule kuendelea kujenga nidhamu katika shule wanazoziongoza katika kuendelea kujenga heshima ya chama.

Chongolo pia ameahidi awamu ijayo watatoa zawadi kulingana na kiwango cha ufaulu katika shule husika na kuwataka walimu kujitahidi katika ufundishaji.

Rais akataa ombi la Waziri Mkuu kujiuzulu
Viongozi wa dini 'chachu' kasi ya chanjo Uviko-19