Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Saed Kubenea amesema kuwa hatarajii kuhama chama chake na kujiunga na CCM kwasababu haendani na chama hicho.

Amesema kuwa hana ugomvi wowote na kiongozi yeyote ndani ya chama chake, hivyo ataendelea kulitumikia jimbo lake la Ubungo mpaka pale itakapomalizika miaka yake mitano.

Kubenea amesema baada ya miaka yake mitano ya kuliongoza jimbo la Ubungo kukamilika atajitathmini na kujipima kama atataka kugombea tena jimbo hilo.

“Mimi sina ugomvi wowote na kiongozi yeyote ndani ya Chadema na sitarajii kuhama Chadema, lakini ikumbukwe hata mimi ni Mtanzania nina uhuru wa kutoa maoni, sijawahi kuongea na kiongozi yeyote wa CCM kuhusu kujiunga na chama hicho,”amesema Kubenea

Hata hivyo, Kubenea ameongeza kuwa ndani ya chama chochote cha siasa lazima kuwepo na mawazo ambayo yanakinzana ili kiweze kusonga mbele.

 

 

Ligi ya mabingwa Ulaya 2018/19
Lionel Messi ajiondoa timu ya taifa