Katika hali isiyokuwa ya kawaida inayozidi kujitokeza katika upambanaji wa vita dhidi ya dawa za kulevya, Kamishna Mkuu wa Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya amesema kuwa, wafanyabiashara hao ni hatari na wana uwezo mkubwa wa kufanya chochote.
Sianga amesema kuwa kazi ya kuusambaratisha mtandao wa biashara hiyo ni kubwa na kadri muda unavyzidi kwenda inazidi kuwa hatari zaidi kwani wafanyabiashara hao wanazidi kubuni mbinu mbalimbali za kukwamisha vita hiyo.
“Wanaofanyabiashara hii wanauwezo wa kufanya chochote wanachotaka, kabla jamii haijatuhukumu ni vyema ikatambua kuwa tunachangamoto kubwa, lakini sisi hatutarudi nyuma tunaendelea kuwakamata mpaka sasa tumewakamata vianara 15, ni watu wenye jeuri ya pesa,”amesema Sianga.
Hata hivyo, ameongeza kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya wanaabudiwa na jamii na kuonekana ni watu wema na wengine ni wafadhili wakubwa ndani ya makanisa na kwenye jamii, pia hubeba jukumu la kugharamia misiba kwenye jamii wanazoishi.