Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt, Dotto Biteko amewataka Wanachama wa Chama cha Mapinduzi – CCM, kufanya siasa za kubadilisha maisha ya watanzania, ili kuwaletea maendeleo badala ya kufanya siasa za maneno matupu zisizojibu hoja na kuleta mabadiliko kwenye jamii.
Dkt, Biteko aliyasema hayo wakati wa mkutano maalum wa jimbo la Chalinze uliopokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2023, ukihudhuriwa na wanachama wake akiwemo Rais Msfafu wa awamu ya nne Dkt, Jakaya Mrisho Kikwete na Mbunge wa Jimbo hilo, Ridhiwani Kikwete.
Amesema, wakati umefika kwa Wanasiasa wa CCM kujibu kwa hoja kutokana na mafanikio makubwa yanayofanywa na Serikali kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020-2025 inayotekelezwa kwa vitendo.
“Niwahase sana watumishi wa Umma kuwahudumia wananchi na kuwafuata walipo pasipo kuwasubiria walete kero zao kwenye madawati, maofisini au kusubilia viongozi wanapo fanya ziara ndipo watatue kero za wananchi ili hali nyie mpo mnalipwa mishahara na serikali ili kuwahudumia wananchi”. Alisema Dkt, Biteko.