Kuwa mjamzito ni kitu cha furaha sana kwa wengine huona ama ni baraka kutoka kwa muumba wetu lakini muda mwingine huongeza upendo na furaha ingawa wachache huwa kama ajali na hupatwa na huzuni tofauti hizi hutokana na mipango ya wanawake hao, hali zao za kimaisha na maandalizi yao.

Baada ya kupata ujauzito kazi kubwa iliyopo mbele ni kulea vizuri ujauzito huo hadi kujifungua mtoto.

Yafuatayo ni mambo hatarishi kwa afya ya mama mjamzito na mtoto aliyeko tumboni ambayo mama mjamzito anaiyajika kujiepusha nayo.

Jambo la kwanza ni kuepuka kuvuta sigara,kunywa pombe, na kutumia madawa ya kulevya hii ni hatari kwa afya yako na mtoto.

Lakini pia matumizi mabaya ya dawa zisizoruhusiwa kwa wajawazito na vipodozi visivyo salama, kuacha kuvaa nguo za kubana na viatu vyenye visigino virefu.

Inashauriwa mama mjamzito asifanye kazi ngumu asiwe na msongo wa mawazo kubwa zaidi hatakiwi kukasirika mara kwa mara na kuhakikisha anakuwa na furaha muda mwingi.

Aidha anatakiwa kuepuka jua kali, vumbi, na kukaa karibu na wanyama wafugwao nyumbani na mabanda yao.

Mjamzito pia aepuke vyakula visivyopikwa na kuiva vizuri kwani vinaweza kukusababishia magonjwa na pia ajiepushe na ugomvi.

Bilioni 800 Kukarabati Barabara Geita
Vyuo vya elimu ya juu vyatakiwa kusimamia maadili