Wanasema ‘like father like daughter’, ni nyota ya ustaa iliyopenya kwenye damu ya mtoto wa Diamond Platinumz, Tiffah mwenye umri wa siku moja tu kufikia leo.

Mtoto huyo tayari ameshakuwa maarufu kwenye mitandao ya kijamii akifikisha followers zaidi ya 44,000 kwenye Instagram, na amepata ombi la kuwa balozi wa duka moja la watoto jijini Dar es Salaam.

Ripoti za kupokea ombi la ubalozi iliwekwa kwenye Twitter na meneja wa Diamond anayefahamika kwa jina la Sallam.

“Leta proposal yako.. Maana nimesema nifungue e-mail nione kuna booking za show naona Proposal ya Ubalozi kwa #Tiffah,” alitweet Sallam.

 


Muda mfupi baadae Sallam alitweet akisema kuwa tayari wameshakubaliana na mmiliki wa duka moja la watoto na anaelekea kusaini mkataba, Tiffah amepata ubalozi.
“Tiffah ndani ya masaa apata Endorsement na duka la watoto naenda kukamilisha Terms na wahusika nitarudi na habari kamili..” alitweet Sallam.

Diamond, Zari na Tiffah hivi inakuwa familia ya mwanamuziki inayofuatiliwa zaidi Afrika Mashariki.

Man Utd Kumjua Mpinzani Wake Leo
Mbatia Asema Yake Baada Ya Profesa Lipumba Kung’atuka Uenyekiti CUF