Ikiwa leo (Oktoba 16, 2022), ni Siku ya Chakula Duniani, bado takribani watu milioni moja wanaishi kwenye mazingira ya baa la njaa, ambapo wengi wao hukosa chakula na kifo ni jambo la kawaida kila uchao kwenye maeneo mbalimbali wanayoishi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres amesema maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika wakati ambapo Dunia inakabiliwa na janga kubwa la uhakika wa kupata chakula na watu wake walio wengi wanazidi kuangamia kwa kukosa maradhi mbalimbali.

Amesema, “Ni janga kwa sababu idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa imeongezeka maradufu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita na kama hiyo haitoshi watu bilioni 3 hawana uwezo wa kupata mlo wenye lishe bora, ikimaanisha wako hatarini kukumbwa na utapiamlo au utipwatipwa.”

Mtama, zao la chakula likiwa shambani. Picha: WFP.

Guterres ameongeza kuwa, “Jamii zilizo hatarini zaidi zinakabiliwa na janga la Uviko-19, madhara ya mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira, mizozo na kuzidi kuongezeka kwa kiwango cha ukosefu wa usawa na vita nchini Ukraine imechochea kasi ya ongezeko la bei ya vyakula, nishati na mbolea.”

Hata hivyo, inahisiwa kuwa kwa baadhi ya maeneo wakati wengine wakikosa chakula, wapo watu wanaoshindwa kupata soko ili kuwea kumudu kuyaendesha maisha yao kutokana na hali ngumu ya maisha iliyosababisha uchumi wa wengi kuyumba, wakiwemo wakulima, walaji na wafanyabiashara.

Wadau wazindua uchunguzi udumavu wa Watoto
Rais Samia 'amkubali' Waziri wa Madini