Rais John Magufuli anatarajiwa kupokea kijiti cha Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa Dkt. Jakaya Kikwete, mwezi Juni mwaka huu.

Dkt. Kikwete ambaye jana alimtembelea Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam anadaiwa kutaka kukabidhi uenyekiti wa chama hicho kwa mujibu wa katiba ya Chama ili aendelee kuwa mwanachama wa kawaida na kiongozi mstaafu.

Kadhalika, imeelezwa kuwa baadhi wa wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wamegawanyika katika mpango huo wa kukabidhiana madaraka huku wengine wakitaka Rais Magufuli apewe uenyekiti mwaka 2017 ili apate muda wa kukisoma vizuri chama na kuwa na uzoefu kwa kuwa hajawahi kushika uongozi wa ngazi yoyote ya chama.

Kundi lingine linataka rais Magufuli akabidhiwe haraka uenyekiti ili aanze kukinyoosha chama hicho mapema kwa kutumbua majipu kama anavyofanya kwenye nafasi yake ya urais.

Baada ya kushinda, Rais Magufuli aliahidi kuwashughulikia wasaliti ndani ya chama hicho bila kuwaonea haya na aliwataka wajisalimishe mapema wenyewe. Hali hiyo imeelezwa kuwatia hofu baadhi ya wananchama.

Taarifa rasmi kutoka Ikulu ilieleza kuwa jana Dk. Kikwete alimpongeza rais Magufuli kwa uongozi wake na kumtakia heri ya mwaka mpya. Taarifa hiyo ilieleza kuwa Dk. Kikwete amesema kuwa anaunga mkono juhudi za rais Magufuli hususan katika kukusanya kodi.

 

Watano wamgomea Magufuli
Mtoto wa Karume amshauri Dk. Shein Ampishe Maalim Seif