Mashabiki na Wanachama wa Young Africans wanaendelea kuminika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kwa ajili ya kupata Burudani mbalimbali sambamba na kushuhudia mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki kati ya timu yao dhidi ya Mabingwa wa Kihistoria wa Afrika Kusini Kaizer Chiefs.

Leo Jumamosi (Julai 22) Young Africans inahitimisha Wiki ya Mwananchi kwa kufanya Tamasha la ‘Siku ya Mwananchi’, ambayo hutumika kutambulisha wachezaji wapya wa Klabu hiyo waliosajiliwa kwa msimu mpya wa Michuano mbalimbali.

Tangu asubuhi Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo Kongwe katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati walianza kuingia Uwanjani hapo, lakini muda unavyozidi kusogea, wameendelea kumiminika kwa wingi.

Mbali na mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs, katika Tamasha hilo la ‘Siku ya Mwananchi’ linanakshiwa na Burudani mbalimbali kutoka kwa Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya pamoja na matukio mengine ya kufurahisha.

Ahmed Ally: Hatubahatisha usajili 2023/24
Mshambuliaji Simba SC aibukia Ihefu FC