Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana kwa siku ya tatu leo kujaribu kufikia makubalino ya mpango mkubwa wa kufufua uchumi kufuatia majadiliano ya siku mbili mjini Brussels kumalizika jana bila kuwepo muafaka.

Viongozi wa kanda hiyo wamesalia kwenye mkwamo kuhusu mpango huo wa uokozi wa baada ya janga la COVID-19 kutokana na upinzani wa mataifa yanayotajwa kuwa “bahili” yakiongozwa na Uholanzi pamoja na washirika wake Austria, Denmark, Finland na Sweden.

Baadaye leo, rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Ulaya Charles Michel anatarajiwa kuwasilisha pendekezo jingine kwa viongozi wakuu 27 wa nchi wanachama baada ya mpango wake wa Euro bilioni 750 kukataliwa na mataifa tajiri ya kanda hiyo.

Mapendekezo mapya yatapunguza kidogo kiwango kilichotengwa kwa ajili ya misaada na kuongeza kiwango cha fedha kwa ajili ya mikopo inayopaswa kurejeshwa na mataifa yatakayonufaika na mpango wa uokozi.

Bil. 20 zatolewa kulipa madeni ya korosho Mtwara
DC Musoma kufunga shule kwa kukithiri vitendo vya kishirikina