Jopo la Madaktari wa Simba SC linasubiriwa kutoa taarifa rasmi kuhusu Kiungo kutoka nchini Uganda Thadeo Lwanga, ambaye anasumbuliwa na majeraha ya goti kwa muda mrefu.

Lwanga hivi sasa anajadiliwa na baadhi ya viongozi kwa kile kilichoelezwa kukaa nje ya uwanja kwa msimu mzima kutokana na majeraha ya goti anayoyauguza.

Simba SC hivi sasa inahusishwa na mpango wa kuwa kwenye mazungumzo na kiungo kutoka nchini Brazil Gerson Fraga kwa ajili ya kuja kuchukua nafasi ya Lwanga.

Taarifa kutoka ndani ya Simba SC zinaeleza kuwa Uongozi bado haujapokea ripoti ya usajili kutoka kwa kocha, Franco Pablo hivyo mara baada ya kuikabidhi itajulikana.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa majeraha ya Lwanga ni ya kitabibu, hivyo Uongozi unasubiria ripoti ya daktari kwa ajili ya kuona muda gani atakaa nje ya uwanja.

Alipoulizwa Daktari Mkuu wa timu hiyo, Yassin Gembe kuzungumzia hilo alisema kwa kifupi: “Mimi sipo na timu, ninaumwa.”

Simba SC kutua Zanzibar Januari 04
Ibenge mdomoni mwa Simba SC Kombe la Shirikisho