Kenya Mwanaume mmoja, Alexander Kerue mwenye umri wa miaka 35 amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mkewe Doris Thogori mnamo October 26 mwaka 2015 katika mahakama kuu ya Nanyuki.

Mahakama imethibitisha kuwa Mwanaume huyo alimuua mkewe mbele ya watoto wao wawili.

Chanzo cha ugomvi baina ya wawili hao ni baada ya kuzozana na hatimaye mwanamke huyo kumuita mumewe ‘Kihii’ yaani Asiyetahiriwa ndipo hasira zikamjaa Mwanaume huyo na kupelekea mauaji hayo.

Wakili Mary Kasango ambaye ni msoma mashtaka amelaani kitendo hiko na kukiita ni kitendo cha kinyama.

Watoto wa mama mazazi aliyeuwa walikuwa mashahidi wa tukio zima na kuiambia mahakama mkasa mzima kuwa baba yao alikuwa akigombana na mama yao, muda mfupi baade walishuhudia baba yao akiwa ameshika kisu huku mama yao akiwa ameanguka chini akiwa na majeraha ya kisu mwili mzima, hali ambayo iliashiria baba yao alimchomachoma visu mama yao na kusababishia kupotezea maisha.

Mtuhumiwa huyo alijitetea na kusema mke wake aliangukia kisu ambacho alikuwa amekishika, ushahidi ambao majaji waliukataa lakini pia Dakatri aliyemtibia alitoa ripoti iliyosema majeraha aliyonayo marehemu hayakuwa ya ajali kama ambavyo mtuhumiwa amedai.

Hivyo Alexander amehukumiwa hukumu ya kifo.

 

Mahakama yatengua kauli zuio la kuapisha wabunge wapya CUF
Washikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za ujambazi