Wachezaji wa Azam Fc kutoka nchini Ivory Coast, Kipre Tchetche na mlinzi Serge Wawa Pascal wameungana na Brien Majwega raia wa Uganda, Kipre Bolou wamejiunga na wachezaji wenzao katika mazoezi ya kujiandaa na michuano ya kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza katikati ya mwezi huu.

Tchetche na Wawa wamewasili wikiendi hii, Majwega aliyekuwa akisumbuliwa na malaria na homa ya matumbo sasa amepona kabisa. Wote kwa pamoja, wataungana na wachezaji wenzao katika mazoezi hayo ya Jumatatu.
Kocha wa Azam Stewart Hall alisema, “Jumatatu natarajia kuwa na wachezaji wangu wote na watakaokosekana ni wale tu waliokuwa na Taifa Stars.”

“Tchetche, Wawa wameshawasili, Majegwa aliyekuwa mgonjwa Erasto Nyoni aliyekuwa na Stars wote wataanza mazoezi na wenzao.” pia wapo baadhi waliokuja kusaka nafasi ya kusajiliwa. Jumanne Azam FC itacheza na JKT Ruvu katika mchezo wa kirafiki

Breaking News: Daniel Yona Na Bazil Mramba Wafungwa Jela
De Gea Kuhudhuria Mazoezi Ya Man Utd Hii Leo