Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, David Silinde amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinasimamia kikamilifu miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri zao ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati.

Ametoa agizo hilo, leo kwenye ziara yake ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

Pia amepongeza usimamizi mzuri uliofanywa na Halmashauri hiyo kwa usimamizi wa ujenzi wa kituo cha afya Mazwi  ambacho kwa sasa kimeanza kutoa huduma kwa jamii.

Dkt. Gwajima awataka Viongozi Wizara ya Afya kuongeza ufanisi

“Nimeridhishwa na ujenzi wa Kituo cha afya cha Mazwi, kimejengwa vizuri na thamani ya fedha na majengo inaonekana, toenihuduma bora za afya kwa jamii ili waweze kuvutiwa na huduma zinaotolewa katika vituo vilivyokarabatiwa na kujengwa na Serikali” amesema . Silinde

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha fedha zinazotolewa zinaenda sambamba na thamani ya miradi inayotekelezwa katika Halmashauri, hivyo ni vyema kuhakikisha zinasimamia kwa karibu ukamilishaji wa miradi yote ili ianze kutoa huduma kwa kwa wakati uliokusudiwa na Serikali.
Wanataaluma Sekta ya Afya wapewa Miezi 6 kujisajili

Wakati huohuo Mgannga Mkuu wa Manispaa ya Sumbawanga Dkt. Archie Hellar amesema Kituo cha Mazwi ni miongoni mwaa vituo 44 vilivyopata kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

 
Aidha, David Silinde akiwa Mkoani Rukwa amekagua  mradi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Uchile,


Hitimana Thiery kocha mpya Mtibwa Sugar
Katwila kuipamba Ihefu FC dirisha dogo