Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa madarasa katika mkoa wa Iringa ma kuwataka waongeze kasi ya kuharakisha ukamilishwaji wa vyumba hivyo huku wakizingatia ubora wa majengo na thamani halisi ya fedha ionekane.
Hayo ameyasema baada ya kutembea ujenzi wa vyumba vya madarasa katika halmshauri Tano (kilolo,manispaa ya iringa,iringa vijijini,mufindi na mafinga) na kukuta ni halmashauri mbili za mufindi na mafinga zilizokamilisha ujenzi katika ubora wa hali ya juu kwa vyumba vyote zaidi ya 80 walivyopewa na kukabidhi mkoani kwa ajili ya kupokea wanafunzi wapya.
Aidha Naibu Waziri Silinde amemuagiza Afisa elimu mkoa wa Iringa Joyce Baravuga kuongeza ufatiliaji katika sehemu zote ambazo bado wapo nyuma katika ujenzi kwani siku walizoongezewa zimebaki chache na ikiwezekana wafanye kazi usiku na mchana waweze kukamilisha lakini wazingatie ubora kwani amegundua katika shule moja ya Kalenga ubora wake haujamridhisha upo chini ya kiwango hivyo wafanye vizuri zaidi ikiwezekana wakawaige watu mufindi wamewezaje kufanya vizuri zaidi.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule amesema sababu kubwa ya wao kufanya vizuri katika ujenzi wa madarasa na kukamilisha kwa wakati na ubora unao takiwa ni kufanya kazi kwa pamoja kama timu kutoka juu mpaka chini kwa kushirikiana kwa kila jambo na wameweza kuchukua mda mdogo wa ujenzi wa mwezi mmoja kwa kufanya kazi usiku na mchana hata ilipobidi gari ya mkuu wa wilaya ilitumika kumilika ili kazi ifanyike na wanahakika wanafunzi wote watasoma.