Naibu waziri ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde ameagiza halmashauli ya Jiji la Dar es salaam na wakala wa Barabara za mjini na Vijijini TARURA wafanye taasmini ya haraka na kutafuta fedha kujenga daraja katika barabara ya mtaa wa sokoine kimanga baada ya wananchi kupata shida kutumia barabara hiyo hasa wakati wa mvua kujaa maji na kushindwa kupitika.

Hayo ameyaeleza akiwa ziara katika jimbo la Segerea kukagua ubovu wa barabara za ndani ya jiji la Dar es salaam na kukuta barabara hiyo haitumiki kwasasa kwani daraja ambalo hutumika limeharibiwa na mvua na kuhatarisha maisha ya wananchi wa maeneo hayo na kuwaletea tabu kuvuka kwenda upande wa pili kufata mahitaji.

Aidha Naibu Waziri Silinde ametoa miezi miwili daraja hilo lianze kujengwa na atafika kukagua utekelezaji wake na sasa si muda wa kubishana bali wafanye tathimini gharama za ujenzi na ujenzi uanze mala moja iwe wakati wa mvua au jua sababu daraja hilo lina maitaji makubwa zaidi.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la segerea Bonnah Kamol amemuomba Naibu Waziri Silinde kupata barabara katika jimbo lake kwani wamesahulika kabisa na barabara nyingi hazipitiki vizuri hivyo wanaomba kukumbukwa katika bajeti itakayokuja kupelekewa barabara nyingi za rami katika mitaa ilinkuwasaidia wananchi wa jimbo la segerea.

Kwa upande wake mwananchi wa mtaa Sokoine Twaha Saidi amemuambia Naibu Waziri kua kwasasa barabara hiyo nikuanganisho kwao lakini imegeuka kua hatari kwani mpaka sasa yeye aameokoa watoto zaidi ya wawili ambao walisombwa na maji wakati wa mvua wakijalibu kuvuka katika mto ambao unapita katika Barabara hiyo hivyo wanaomba serikali kuwasaidia kuwajengea daraja kubwa zaidi ambalo maji yatapita vizuri n akuwatengenezea barabara ipitike.

Bidhaa zenye thamani ya millioni 200 zakamatwa
Ajibadilisha sura afanane na paka kumfurahisha mumewe