Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitaka Idara ya Kazi, Ofisi ya Waziri Mkuu kusimamia mpango wa urithishwaji wa ujuzi kwa wazawa kama ilivyobainishwa katika Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini.

Rais Samia alitoa tamko hilo mara baada ya ufunguzi wa kiwanda cha kutengeneza vioo cha Sapphire Float Glass na kudai kuwa mpango huo utawasaidia Watanzania wengi kupata ujuzi na ajira na kumsaidia mwekezaji kupunguza gharama za kuajiri wataalamu wa kigeni.

Amesema, Serikali inaendelea kuwekeza kwenye mifumo ya utoaji huduma ili kupunguza urasimu na kutekeleza hatua za kiuchumi huku akidai kuwa Serikali pia inatarajia kuzindua Mfumo wa kielektroniki wa kuhudumia wawekezaji, ambao utaunganisha taasisi 12 za Serikali zinazotoa huduma kwa wawekezaji.

Aidha, Rais Samia pia amesema wawekezaji watakaotaka kuwekeza nchini watapewa msaada katika mchakato wa usajili wa kampuni, upatikanaji wa ardhi, vibali na leseni kupitia dirisha moja la huduma ndani ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania – TIC.

Makala: Mtaala Lugha ya Alama ulete ufanisi kwa Kiziwi
Uamuzi wa Mahakama wasababisha raia kupigwa marufuku