Kocha wa Simba, Jackson Mayanja anatarajiwa kuwasili leo ama kesho, tayari kwa maandalizi ya kikosi chake ambacho msimu ujao wa ligi kinatarajiwa kufanya makubwa zaidi ya ilivyokua msimu wa 2015-16.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema mara Mayanja atakapowasili, wachezaji wote wenye mikataba na klabu hiyo wakiwemo wapya ambao wamesajiliwa hivi karibuni wataanza mazoezi.

Poppe amesema kwamba kutakuwa na programu ya awali itakayofanyika jijini Dar es Salaam na mara baada ya kikosi kizima kukakamilika, timu itakwenda kuweka kambi rasmi ya kujiandaa na msimu mpya katika mkoa ambao utatajwa baadaye.

Kuhusu kocha mpya, Poppe amesema suala hilo bado linafanyiwa kazi na Kamati ya Ufundi, chini ya Mwenyekiti wake, Collin Frisch na mara litakapokamilika litawekwa wazi.

Korea kaskizini kuichokoza Korea kusini tena
Real Madrid Wasalimu Amri, Wakubali Kumrudisha Morata