Kikosi cha Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika Simba SC, kinatarajia kuondoka Dar es salaam kesho Ijumaa (Februari 18), kuelekea Niger tayari kwa mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya US Gendarmerie.
Mchezo huo wa Mzunguuko wa pili wa Hatua ya ‘Kundi D’ utachezwa mjini Niamey kwenye Uwanja wa Général Seyni Kountché Jumapili (Februari 20), saa moja jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Simba SC itaingia Dimbani huku ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast Jumamosi (Februari 13), Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.
Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema mipango ya safari ya kuelekea Niger imeshakamilika na wanatarajia wakiwa huko watapambana na kuendeleza wimbi la ushindi, licha ya kutambua wapinzani wao watahitaji kushinda nyumbani.
“Tutaondoka hapa Februari 18 kuelekea Niger, kila kitu kimeshawekwa sawa na viongozi wetu, tunaamini tukiwa huko tutapambana ili kuendeleza mazuri kimataifa.”
“Tunaamini mchezo utakua mgumu, Wapinzani wetu wamepoteza mchezo wao wa kwanza, hivyo watahitaji kupambana vilivyo wakiwa nyumbani na kupata alama tatu. Simba SC itakua katika hali kama hiyo, jambo ambalo linaendelea kuongeza chachu ya upinzani katika mchezo huo.” Amesema Ahmed Ally.
Katika Msimamo wa ‘Kundi D’ Simba SC ina alama 3 sawa na RS Berkane ya Morocco, huku ASEC Mimosas (Ivory Coast) na Kikosi cha Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika Simba SC, kinatarajia kuondoka Dar es salaam kesho Ijumaa (Februari 18), kuelekea Niger tayari kwa mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya US Gendarmerie (Niger) zikiwa katika nafasi mbili za mwisho.