Wachezaji watano wa Simba Sc akiwemo Henock Inonga na Clatous Chota Chama na Wengine 3 (hatujayapata majina yao) wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi yao baada ya kufungwa na Yanga SC mabao 5-1 siku ya Jumapili.
Wachezaji hao wanatuhumiwa kuihujumu timu kitendo kilichopelekea kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao
Maamuzi hayo yamefanyika katika kikao cha bodi ya Wakurugenzi ya Simba kilichofanyika jana jijini Dar es salaam
Wachezaji hao 5 watakua nje ya kambi ya timu mpaka hapo maamuzi mengine yatakapofanyika
Chanzo hicho kimesema huwenda leo klabu ya Simba ikatoa taarifa ya wazi kwa Umma juu ya maamuzi waliyofikia kuhusu wachezaji hao au wasitoe ila wahusika wamepewa taarifa.