Klabu za Coastal union na Simba SC zitavaana tarehe 11 agosti katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu wa michuano ya ngao ya jamii itakayopigwa Saa 9 alasiri jijini Dar es salaam dimba la Benjamin mkapa.

Simba ilishindwa kutinga fainali za michuano hiyo baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Yanga bao lililofungwa na Max Nzengeri dakika ya 44.

Coastal union walishindwa kufika fainali za michuano hiyo baada ya kukubali kipigo cha mabao 5-2 kutoka kwa Azam FC.Mabao ya mchezo huo yalifungwa na Gibril Silla ,Feisal salum,Blanco,meza na Adam Adam.

Mchezo unaosubiriwa kwa hamu ni fainali ya Azam FC Vs Yanga. Mchezo huo utapigwa majira ya Saa 1 usiku katika dimba hilohilo la Benjamin mkapa. Hii inakuwa ni mara ya Kwanza kihistoria kwa klabu za Simba na Yanga kuutumia uwanja wa Benjamin mkapa siku moja kwa mechi tofauti.

Kilele cha mechi hizo ni ufunguzi rasmi wa ligi kuu ya NBC kwa msimu wa 2024/25 na mechi ya Kwanza itapigwa jijini Mwanza katika dimba la CCM kilumba ikizikutanisha Pamba JIJI dhidi ya Tanzania Prisons.

 

Simulizi: Sina hamu na Ukahaba
Hii hapa ratiba ya ligi kuu NBC msimu wa 2024/25