Kikosi cha Simba Queens kinatarajia kutua Dar es salaam keshokutwa Jumatano (Novemba 16) kikitokea Morocco ambako kilikua kinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake.
Simba Queens inarejea nchini ikiambulia nafasi ya nne kwenye Michuano hiyo iliyoshiriki timu nane kutoka pande zote za Bara la Afrika.
Meneja wa Simba Queens Seleman Makanya amesema kikosi kitawasili majira ya saa tisa usiku na kitapokelewa na Wapenzi na Wanachama wa klabu hiyo.
“Tunatarajia kutua nyumbani Tanzania saa tisa usiku wa siku ya Jumatano.”
“Nafikiri hadi kumaliza utaratibu wa ukaguzi hadi kufikia alfajiri tutakuwa tunatoka.” amesema Makanya.
Simba Queens ilipangwa Kundi A sambamba na Wenyeji AS FAR Rabbat (Mabingwa), Green Buffaloes ya Zambia na Determine Girls ya Liberia.
Kundi B lilikua na timu za Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Nigeria Bayelsa Queens (Nigeria), TP Mazembe (DR Congo) na Wadi Degla (Misri).