Mabingwa wa soka Tanzania Bara na wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Simba SC, Wanasubiri droo itakayopangwa kesho Ijumaa Januari 8 mjini Cairo, Misri.

Simba imefika hatua hiyo baada ya kushinda mabao manne kwa sifuri  dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe jana Jumatano (Januari 06), licha ya kufungwa bao 1-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa mjini Harare, Desemba 23 mwaka 2020.

Wakiwa wanasubiri droo, Simba SC wamepangwa kwenye chungu (Pot) cha tatu na timu za El Hilal ya Sudan, Petro de Luanda ya Angola na MC Alger ya Algeria.

Kwa mantiki hiyo Simba SC watapangwa kundi moja na timu kutoka kwenye vyungu (Pots) namba moja, mbili na nne.

Ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya Makundi:

·Mzunguuko wa Kwanza – Februari 12/13

·Mzunguuko wa Pili  – Fabruari 23

·Mzunguuko wa Tatu– Machi 5/6

·Mzunguuko wa Nne – Machi 16

·Mzunguuko wa Tano– Aprili 2/3

·Mzunguuko wa Sita– April 9/10

Simba yaachana na kocha Sven
Yondani ampa jeuri Kocha Polisi Tanzania FC

Comments

comments