Tanzania itakuwa mwenyeji wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya African Super League ambayo yamebadilishwa jina na sasa yanatambulika kama ‘African Football League’.

Mashindano hayo mapya ya kuwania ligi ya bara Afrika, itakayoshirikisha timu nane, rasmi yataanza Oktoba 20, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kwa kuwahusisha wenyeji Simba SC dhidi ya timu itakayotajwa hapo baadae.

Awali, timu 24 zilitarajiwa kushiriki kwenye michuano hiyo, lakini idadi imepunguzwa, wakati CAF ikitangaza hasara ya Dola Milioni 15.7 kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Rais wa FIFA Gianni Infantino, alitangaza maamuzi ya tarehe rasmi ya kuanza kwa michuano hiyo kupitia Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ uliofanyika mjini Abidjan, Ivory Coast jana Alhamisi (Julai 13).

” Michuano hii itakuwa na timu nane kubwa, ambazo zitafuatwa katika siku zijazo kwa toleo kubwa,”

“Tunapaswa kuwekeza katika soka la vilabu vya Afrika pamoja na soka la timu za taifa za Afrika.”

“Ni jukumu letu, na mchango wetu sisi kama wadau wa soka duniani, ninaamini tutafanikiwa.” Infantino aliwaambia wajumbe wa mkutano mkuu wa CAF.

Rais wa FIFA  Gianni Infantino

Timu nane zitakazoshiriki michuano hiyo ni Mabingwa wa Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns, ambao wanamilikiwa na familia ya Rais wa ‘CAF’ Patrice Motsepe, Petro Atletico (Angola), TP Mazembe (DR Congo), Al Ahly (Misri), Horoya (Guinea), Wydad Casablanca (Morocco), Simba (Tanzania) na Esperance (Tunisia).

Mashindano hayo yataenda sambamba na Michuano ya Ligi ya Mabingwa ya mabingwa, na Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu wa 2023/24.

“Tumetambua kwa miaka mingi kwamba wachezaji wa kandanda wa Afrika wamekuwa miongoni mwa wachezaji bora zaidi duniani, lakini tunapaswa kuboresha mvuto wa soka la Afrika, uwezo wake wa kibiashara na uwezo wake wa kujiendeleza,” alisema Rais wa CAF Motsepe akiwaambia wajumbe wa mkutano mkuu wa CAF.

Rais wa CAF Motsepe (Katikati) akiwa na Rais wa FIFA Infantino (Kushoto) na Katibu Mkuu wa CAF Véron Mosengo-Omba (Kulia)

CAF pia ilithibitisha hasara kwa mwaka uliopita wa fedha, lakini hiyo ni nyuma ya uboreshaji wa mapato ya 17% hadi Dola 125.2 milioni, ambayo wanatarajia itapanda zaidi katika mwaka wa fedha wa 2023-24.

Upungufu huo haukuwa wa kawaida baada ya CAF kupata suluhu nje ya mahakama kwa mtu ambaye hajatajwa na wakala wa kibiashara wa Lagardere Novemba mwaka jana, baada ya kughairi mkataba wa miaka 10, wa dola bilioni 1 wa haki za televisheni na haki za masoko mwaka 2019.

“CAF ilibidi kuchukua maamuzi magumu kuhusu mzozo wa muda mrefu na baadhi ya washirika wetu kwa kutatua masuala nje ya mahakama,” imeeleza taarifa ya CAF iliyowasilishwa katika Mkutano Mkuu.

“Hii ni pamoja na masharti mengine ya viwango vya uhasibu yaliyopendekezwa na wakaguzi wa CAF, yalitolewa kikamilifu katika fedha.”

Maelezo kuhusu watangazaji, wafadhili na vifaa, pia yanabakia kufichwa kwa sasa.

Motsepe amezungumza kwa kirefu katika miaka ya hivi karibuni ya kuhitaji kuboresha ‘bidhaa’ ya soka la Afrika ili kuifanya ivutie zaidi hadhira ya kimataifa, huku ligi mpya ikitajwa kuwa muhimu kwa hilo.

Luis Miquissone atua Simba SC kimya kimya
Kombe la dunia 2026: Tanzania mikononi mwa Morocco