Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC kinaondoka Dar es salaam leo Jumanne (April 06) majira ya saa 9:25 alasiri kwenda nchini Misri kupitia Dubai.

Msafara wa kikosi hicho utakuwa na jumla ya wachezaji 25 ambapo Kitaondoka Dar mpaka Dubai, kitapumzika Dubai na kesho Jumatano (April 07) asubuhi kitaondoka Dubai kwenda Cairo, Misri na kufika saa 4:05 asubuhi.

Simba wanaenda Cairo Misri kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Hatua ya Makundi dhidi ya wenyeji wao klabu ya Al Ahly ya Misri mchezo ambao utachezwa Ijumaa ya (April 09).

Simba SC inaongoza msimamo wa ‘Kundi A’ ikiwa na alama 13, ikfuatiwa na Al Ahly yenye alama 08, huku AS Vita ikishika nafasi ya pili na Al Merrikh inaburuza mka kwa kuwa na alama 02.

Simba SC na Al Ahly zimeshafuzu hatua ya Robo fainali, hivyo mchezo wao wa Ijuma (April 09) utakua ni wa kukamilisha ratiba ya michezo ya ‘Kundi A’.

Al Merrikh wavamia Kinshasa
Gomes: Manula haendi popote