Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed lly, amesema leo Jumatatu (Julai 11) klabu hiyo itamtambulisha mchezaji wa mwisho mzawa aliyesajiliwa katika kipindi hiki, baada ya kumtambulisha Habib Kyombo Jumamosi (Julai 09).

Ahmed Ally amesema mchezaji huyo atatambulishwa rasmi majira ya saa saba mchana kupitia Simba APP na Kurasa za Mitandao ya Kijamii za klabu hiyo, kisha utambulisho mwingine utaendelea kesho Jumanne (Julai 12).

Amesema utambulisho wa kesho na kuendelea utawahusisha wachezaji wa Kimataifa waliosajiliwa klabuni hapo kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

“Leo tutamtambulisha mchezaji wa mwisho mzawa, baada ya kumtambulisha Habib Kyombo ambaye ni mzawa pia, siku ya Jumamosi, kama utakumbuka jana tulimtambulisha Victor Akpan, yeye ni mchezjai wa Kimataifa japokuwa alikua anacheza hapa Tanzania msimu uliopita,”

“Kuanzia kesho Jumanne tutaanza kuwatangaza wachezaji wa kimataifa ambao hawajawahi kucheza soka katika Ligi ya Tanzania, Mashabiki wa Simba wataanza kuona nani ni nani katika usajili wa kimataifa, hatutambulishi watu kwenye mikutano ya uchaguzi sisi.” Amesema Ahmed Ally

Hata hivyo tayari imeshaanza kuhisiwa huenda leo Jumatatu (Julai 11) Simba SC ikamtambulisha Nassor Kapama ambaye anadaiwa kusajiliwa klabuni hapo akitokea Kagera Sugar.

Nabi: Usajili huu roho yangu imetulia
Akpan: Mashabiki wamenileta Simba SC