Katika kuadhimisha miaka 80 tangu Simba ianzishwe, klabu hio imeamua kusherekea siku hiyo kwa kuialika klabu kutoka Angola katika tamasha la siku ya Simba (Simba Day).

Kikosi hicho cha Inter Club kitapambana na Simba katika mchezo wa tamasha la Siku ya Simba ambayo litafanyika Agosti 8, siku ambayo Simba itakua inatimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1936.

Inter Club inanolewa na kocha wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic ambaye aliinoa Simba msimu wa 2014/15 kabla ya kutupiwa virago baada ya kufungwa mabao 3-0 na Zesco United katika tamasha la siku ya Simba.

Wakati huo huo Viongozi na wanachama mbalimbali wa Simba watachangia damu katika hospitali mbalimbali.

Rais wa Simba, Evans Aveva amesema watafanya hivyo ikiwe ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Simba kwenda kusherekea miaka 80 ya klabu hiyo.

Siku kamili ya sherehe itakuwa ni Agosti 8 wakati tamasha la Simba Day litakapofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijiji Dar es Salaam.

“Hii ni kuungana na jamii, tutafanya hivyo katika hospitali mbalimbali ambazo zitatangazwa hapo baadaye,” alisema Aveva.

TFF: Muda Wa Usajili Wa Wachezaji Hautaongezwa
Mtambo wa mawasiliano Kenya washambuliwa