Kikosi cha mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC kesho Jumanne asubuhi (Juni Mosi) kitaondoka kwa ndege kwenda jijini Mwanza, kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting.

Simba SC watakuwa wageni kwenye mchezo huo utakaochezwa siku ya Alhamisi Juni 3, katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Ruvu Shooting wamechagua uwanja wa CCM Kirumba kama uwanja wao wa nyumbani kwa mchezo huo, kufuatia kanuni za ligi kuu kuruhusu kwa kila kitu kuchagua uwanja tofauti na uwanja wao wa nyumbani kwa mchezo usiozidi mmoja.

Klabu nyingine zilizowahi kutumia kanuni hiyo ni KMC FC walipocheza dhidi ya Young Africans mwaka jana katika uwanja wa CCM Kirumba na mchezo huo ulikwisha kwa wenyeji kufungwa 2-1.

Simba SC inaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 64, wakiwa wametoka kuifunga Namungo FC mabao 3-1 mwishoni mwa juma lililopita.

Ruvu Shooting wanashika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Tarimba aichana TFF bungeni
Majaji wapatiwa mafunzo