Klabu ya Al Masry ya nchini Misri ndio mpinzani wa wawakilishi wa Tanzania bara katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Wekundu wa Msimbazi Simba, baada ya kufanikiwa kusonga mbele licha ya kufungwa na Green Buffaloes ya Zambia mabao mawili kwa moja.
Al Masry wamefuzu kwa jumla ya mabao 5-2 baada ya ushindi wao wa mabao 4-0 walioupata majuma mawili yaliyopita wakiwa nyumbani Misri.
Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gendamarie na kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwa idadi ya mabao 5-0.
Kwa mantiki hiyo, Simba inakwenda kukutana na mlima mwingine raundi ya mapema baada ya kurejea katika michuano ya kimataifa.
Mchezo wa kwanza katia ya miamba hiyo utachezwa jijini Dar es Salaam, kabla ya Simba kufunga safari na kwenda Misri kumalizia ngwe hiyo inayotarajia kuwa ngumu