Uongozi wa Simba kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema wamepania kumpa zawadi Aliyekua Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Joseph MAgufuli kupitia michuano ya Afrika kwa kufika hadi hatua ya nusu fainali ama hatua ya fainali.

Simba SC inashiriki michuano hiyo hatua ya makundi  na kwa sasa inaongoza msimamo wa kundi A, lenye timu za Al Ahly (Mabingwa Watetezi) kutoka nchini Misri, AS Vita ya DR Congo na Al Merrikh ya Sudan.

Simba inongoza kundi hilo kwa kuwa na alama 10 huku ikisaliwa na michezo wiwili dhidi ya AS Vita nyumbani jijini Dar es salaam na kisha Al Ahly nchini Misri.

‘Try Again’ amesema wakati wa uhai wa Rais Magufuli Simba ilikua inapokea salamu za pongezi kutoka kwa kiongozi huyo, kila ilipokua inafanya vyema kwenye michezo ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika, tangu walipoifunga Plateau United ya Nigeria.

“Ilikuwa kila akisikia tumeshinda anayekutana naye na kumpa salamu hizo huwa aanamuachia ujumbe akisema kawaambie wamefanya vizuri, ila nataka kuona wanafanikiwa zaidi huko Afrika,”

 “Mnakumbuka aliwahi kutusema tulipofungwa na Kagera Sugar? Ile kwetu ilikuwa kama njia ya kutufanya tujipange zaidi na hakuishia hapo aliendelea kututumia salamu za kututaka tuweke pembeni maandalizi ya zimamoto na tujenge timu ya kweli.”

 “Sasa tunafanya vizuri ndani na hata Afrika, ninachoweza kusema haya ni matunda ya kutuhimiza kwake, tulikaa kama bodi na kusema tuweke nguvu ya kutosha ili tufikie malengo ambayo mkuu wa nchi anayataka,”

 “Tunataka kufanya kitu kwa kumuenzi mchango wake unajua miaka sita hii hakuna klabu ambayo inaweza kupita mbele yetu na kusema imefanikiwa kushinda Simba, tupo katika hatua kubwa ya kufika robo fainali,” alisema Tray Again na kuongeza;

“Ila bodi yetu na klabu kwa ujumla hatutaki kuishia hapo tunataka kufika nusu fainali au ikiwezekana fainali kabisa,tukifika hapo tutaona ni zawadi kubwa kwetu kwa Rais wetu huyu mpendwa ambaye kiukweli amelifanyia makubwa taifa hili.”

Simba SC itaendelea na kampeni ya kusaka alama tatu muhimu kwenye michezo ya ‘Kundi A’ mwanzoni mwa mwezi ujao (April) kwa kucheza dhidi ya AS Vita Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, na kisha itakwenda Misri kumalizia michezo ya hatua ya makundi kwa kupapatuana na Al Alhy.

Simba SC ilifanikiwa kuifunga AS Vita mjini Kinshasa bao 1-0, ksha ikasambaratisha Al Ahly jijini Dar es salaam kwa kuifunga bao 1-0.

Garzitto: Soka la Afrika linanuka rushwa
Bendera ya Umoja wa Mataifa kupepea nusu mlingoti kumuenzi Magufuli