Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, wameendelea kusisitiza utayari wa kuelekea mpambano wa mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar, utaaochezwa Uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro Septemba 12.

Kikosi cha Simba SC, mapema leo asubuhi kilianza safari ya kuelekea mkoani Morogoro tayari kwa mpambano huo, unaotazamwa kama sehemu ya kulipa kisasi kwa wenyeji Mtibwa Sugar, ambao kwa mara ya mwisho walikubali kufungwa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya mabingwa hao mara tatu mfululizo.

Mkuu wa Idara ya habari na mawasilino ya Simba SC, Haji Sunday Ramadhan Manara amesema wachezaji wote wapo fiti na watakapowasili mjini Morogoro, wataendelea na maandalizi ya kuelekea mpambano huo.

 “Tunajiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, taarifa niliyopewa ni kwamba tayari Gerson Fraga yupo Bongo, Ame ambaye alikuwa akisumbuliwa na majeraha naye yupo vizuri na mchezo wetu wa kwanza wachezaji wetu hawajaumia hilo ni jambo zuri.”

“Malengo yetu ili yatimie ni lazima tupate matokeo kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, ili kutimiza lengo la kuendelea kukusanya alama tatu za kila mchezo kwa msimu huu.”

“Tutahakikisha tunafanya hivyo kwa mchezo mmoja baada ya mwingine, tunatambua kwamba ligi ni ngumu, na ushindani ni mkubwa lakini tupo tayari, mashabiki waendelee kutupa ushirikiano.” Amesema Manara.

Tayari Simba SC imeshajikusanyia alama tatu za mchezo wa mzunguuko wa kwanza dhidi ya Ihefu FC uliochezwa mjini Mbeya mwishoni mwa juma lililopita, ambapo mabingwa hao watetezi walichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja yaliyofungwa na nahodha na mshambuliaji John Raphael Bocco na Mzamiru Yassin, huku bao la kufutia machozi kwa wenyeji likifungwa na Omar Mponda.

Picha za kikosi cha Simba kilipokua kinaanza safari kuelekea mkoani Morogoro.

Mugalu na Bwalya.
Bernard Morrison.
Joash Onyango.
Ibrahim Ajibu.
Pascal wawa.
Meddie Kagere.

Jela miaka 30 kwa kubaka mwanafunzi
Nuru ya ushindi yaonekana Young Africans