Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC umepokea kwa mikono miwili ombi la Mwekezaji wa klabu hiyo Mohamed Dewji ‘Mo’ la kutaka Bodi ya Wakurugenzi ikae na kuja na utaratibu wa haraka ili kufanikisha mpango wa ujenzi wa Uwanja wa klabu huyo.
‘Mo’ amewasilisha ombi hilo kwa Bodi ya Wakurugenzi mapema hii leo Jumatatu (Desemba 13), kufautia andiko aliloliweka kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, huku akiahidi kuchangilia Shilingi Bilioni 2.
Muda mchache uliopita Uongozi wa klabu hiyo umejibu kwa kuweka andiko kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za klabu ya Simba SC kwa kuandika: “Tunamshukuru Rais wa Heshima wa Simba kufungua milango ya ujenzi wa uwanja wa Simba. Tumeanza mchakato ambao utawezesha Wanasimba kushiriki kuchangia ujenzi. Hivi karibuni tutawatangazia utaratibu.”
Msukumo wa Simba SC kuhimizana kujenga Uwanja wao ambao utatumika kwa ajili ya michezo ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ umekuja kufuatia kitendo cha Afisa Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez kuzuiwa kuingia Uwanjani Jumamosi (Desemba 11) wakati wa mchezo wa Watani wa jadi.