Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wamejizatiti kupata ushindi kwenye mchezo wa Mzunguuko wa 14 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons.

Simba SC itakua mwenyeji wa mchezo huo kesho Alhamis (Februari 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, saa moja usiku.

Kocha Msaidizi wa Simba SC Seleman Matola amesema kikosi chao kimejiandaa vizuri kuelekea mchezo huo, na wanatarajia kupata matokeo mazuri, baada ya kushindwa kuchomoza na ushindi kwenye michezo mitatu iliyopia dhidi ya Mbeya City, Mtibwa Sugar na Kagera Sugar.

“Ilikua ni kama bahati mbaya kwetu kushindwa kupata ushindi katika michezo mitatu iliyopita, tumejipanga kupambana katika mchezo wa kesho ili kurejesha hadhi ya Simba SC kwenye michuano ya Ligi Kuu.”

“Tanzania Prisons sio timu ya kubeza, tunaiheshimu na kuamini itatoa upinzani mkubwa dhidi ya kikosi chetu, hivyo tumejipanga kuhakikisha tunakabiliana na hilo ndani ya dakika 90.” amesema Matola

Baada ya kupoteza michezo miwili dhidi ya Mbeya City na Kegara Sugar huku ikitoka sare mara nne Simba SC imeachwa kwa alama 10 na Young Africans inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 35.

Kibu Denis kuikosa Tanzania Prisons
Athanas Mdamu kuivaa Simba SC