Klabu ya Simba SC inahusishwa na mpango wa kumuajiri Kocha kutoka nchini Tunisia Radhi Ben Abdelmajid Jaidi, ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Kocha kutoka nchini Brazil Roberto Oliviera ‘Robertinho’.

Simba SC imekuwa katika mchakato wa kumsaka Kocha Mkuu kwa majuma mawili sasa, na tayari inatajwa kufanya mazungumzo makocha Sven Vandenbroeck (Ubelgiji) na Abdelhak Benchikha (Algeria) na sasa inatajwa kuhamia kwa Jaidi.

Hata hivyo Uongozi wa Simba SC umekuwa ukisisitiza kuwa, Kocha Mkuu wa kikosi chao huenda akatangazwa kabla ya mchezo wa Mzunguuko wa kwanza wa Kundi B wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Jumamosi (Novemba 25).

Kocha Jaidi anayetajwa kuwa katika mazungumzo na Uongozi wa klabu hiyo kwa sasa, alizaliwa Agosti 30, 1975, na aliwahi kuitunmikia timu ya taifa ya Tunisia akicheza beki wa kati.

Alianza kucheza soka katika ngazi ya vijana akiwa na Stade Gabesien na Esperance zote za Tunisia kati ya 1988-1993 kabla ya kuichezea Esperance ya wakubwa kati ya 1993-2004 na kutua Bolton Wanderers, Birmingham City na Southampton zilizowahi kutamba Ligi Kuu ya England kisha kugeukia ukocha na kuanza 2013 na kufundisha timu za vijana ya Southampton za U21 na U23 kati ya 2014-2017.

Kocha huyo mwenye leseni ya UEFA Pro, anapenda kutumia mfumo wa 4-3-3, 3-4-3, 3-4-2-1, 4-2-2-2 na 3-5-2. Amewahi pia kuwa Kocha Mkuu wa Hartford Athletic inayoshiriki Ligi ya Marekani (USL Championship) huku akiwa pia kocha msaidizi wa timu ya Cercle Brugge ya Ubelgiji kabla ya kutua Esperance ya Tunisia alioachana nao mwaka jana akitoka kuwapa taji la Super Cup kwa kuifunga CS Sfaxien.

Holcim Group yaiweka sokoni Mbeya Cement
Everton hatarini kulimwa Point nyingine