Klabu ya Simba imekataa kuvaa logo ya mdhamini mwenza wa ligi kuu (GSM), CEO wa klabu hiyo Barbara Gonzalez amesema wameandika barua bodi ya ligi kuomba ufafanuzi baada ya kuambiwa kuanzia mchezo ujao wanapaswa kuvaa logo ya mdhamini mwenza wa ligi kuu (GSM)

Kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu Tanzania bara , ukikataa kuvaa logo ya mdhamini unapigwa faini ya Tsh milioni 3 kwa mechi Ukiendelea kukaidi, unashushwa daraja.

Mkataba waliosaini GSM na TFF masharti yaliyopo kutoka GSM ni kuwa, logo yao inapaswa kukaa upande wa kushoto wa jezi, Tayari Simba SC walishapewa logo hizo na mamlaka za soka nchini wazitumie kuanzia mchezo unaofuata wa derby ya Kariakoo.

Simba SC yarejea Dar es salaam
Mtibwa Sugar yaona mwezi Ligi Kuu