Shirikisho la soka nchini TFF limekemea kauli iliyotolewa jana Jumatano (Desemba 02),  na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Simba SC Haji Sunday Manara, ya kuwataka mashabiki wa Young Africans kutokufika Uwanja wa Benjamin Mkapa, kushuhudia mchezo wa mkondo wa pili hatua awali dhidi ya Plateau United ya Nigeria.

TFF imetoa taarifa hiyo kwa kutaka haki na usawa kwa mashabiki wote nchini kuingia viwanjani kwa mujibu wa katiba ya Shirikisho la soka duniani FIFA inayopiga ubaguzi wa aina yoyote.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa mashabiki wote pasina kujali itakazi za ushabiki wao, wataruhusiwa kuingia uwanjani siku hiyo ya mchezo wa Simba SC dhidi ya Plateau United.

“Hata klabu ambazo zinamiliki viwanja hutenga tiketi maalum kwa ajili ya timu pinzani na makundi maalum.” Imeeleza taarifa hiyo.

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limeruhusu asilimia 50 ya mashabiki kuingia uwanjani kushuhudia mchezo wa Simba dhidi ya Plateau United (sawa na mashabiki 30,0000), baada ya kujiridhisha Tanzania haina matatizo makubwa maambuki za virusi vya Corona.

Imethibitishwaa Rihanna na A$AP Rocky kutoka kimapenzi
KMC FC waisuburu kwa hamu Dodoma Jiji

Comments

comments