Uongozi wa Mabingwa wa Soka nchini Uganda Vipers SC umeivimbia Simba SC kuelekea Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu 2022/23.

Simba SC imepangwa Kundi C katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika sambamba na Vipers SC inayoshiriki Michuano hiyo kwa mara ya kwanza, Raja Casablanca (Morocco) na AC Horoya (Guinea).

Afisa Mtendaji Mkuu wa Vipers ya Uganda Simon Njuba amesema wanaiheshimu sana Simba SC kutokana na kuwa Klabu yenye Historia kubwa katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, pia ina uzoefu wa kupambana Kimataifa.

Njuba amesema pamoja na kutoa heshima hiyo kwa Simba SC, haiwaogopeshi kuelekea mchezo wa Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, kwani wapo tayari kupambana na kumaliza kinara ama nafasi ya pili kwenye Kundi C.

Amesema kitendo cha Vipers SC kutinga Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, kimedhihirisha nao ni wakubwa na wapo tayari kukutana na yoyote, na imekuwa bahati wamepangwa na Simba SC, Raja Casablanca pamoja na AC Horoya.

“Simba ni timu kubwa, ni timu nzuri inawachezaji wazuri lakini Vipers SC pia ni timu kubwa ukiona timu iko Hatua ya Makundi Klabu Bingwa ni timu kubwa tumejiandaa kukabiliana nao”

“Tulijiandaa kukutanishwa na yoyote katika Hatua ya Makundi na tulijua hilo kwa sababu tulikuwa miongoni mwa Klabu zilizofuzu hatua ya Makundi, kwa hiyo tutapambana na kufanikiwa.”

“Lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunamaliza kinara wa Kundi C ama nafasi ya pili, ili tuingine Hatua ya Robo Fainali ya Michuano hii, kwa hiyo ninazitaka timu zilizopangwa nasi katika Hatua hii kujiandaa kukabiliana na kikosi chetu.” amesema Njuba

Vipers SC itaanza kampeni ya kutinga Hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kucheza ugenini Uwanja wa Mohammed V dhidi ya Raja Casablanca, kisha itarejea nyumbani mjini Entebe katika Uwanja wa St. Mary’s kwa kupapatuana na Mabingwa wa Soka nchini Guinea AC Horoya.

Mchezo wa Mzunguuko wa tatu Hatua ya Makundi Vipres SC itaendelea kubaki nyumbani katika Uwanja wa St. Mary’s ikicheza dhidi ya Simba SC ya Tanzania na kabla ya kuanza safari ya Dar es salaam kwa mchezo wa Mzunguuko wa nne.

Mchezo utakaofuata Vipers SC itarejea nyumbani katika Uwanja wa St. Mary’s kuikaribisha Raja Casablanca na kisha itakwenda ugenini Guinea katika Uwanja wa General Lansana ContĂ© kumalizana na AC Horoya.

Vipers SC: Simba SC, Young Africans njooni tuzungumze
Azam FC: Tumepokea ofa ya Young Africans