Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wamesema kwa sasa hawafikirii lolote zaidi ya kutafakari namna watakavyopambana na USGN ya Niger katika mchezo wa mwisho wa ‘Kundi D’, Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Simba SC itakua mwenyeji wa mchezo huo Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Jumapili (April 03), huku ikihitaji ushindi wa aina yoyote ili kujihakikishia kutinga hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Meneja wa Habari na Mawasilino ya Simba SC Ahmed Ally amesema kwa sasa Uongozi wa juu na baadhi ya Wanasimba wamekua katika majadilino makali kuhusu mchezo huo, ambao una umuhimu mkubwa sana kwao.

Amesema mipango mingine ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ kwa sasa imewekwa pembeni kwa sababu hakuna cha ziada zaidi ya kuhakikisha wanashinda dhidi ya USGN ya Niger.

“Hakuna kingine ambacho kinatuchukulia muda kwa sasa zaidi ya mchezo wetu dhidi ya USGN ambao tutacheza nao Jumapili (April 03) hapa jijini Dar es salaam, tutahitaji kushinda mchezo huu, ndio maana akili zetu zipo hapo.”

“Kuhusu Ligi Kuu ama Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ hiyo itakua baadae baada ya kumazina na hawa USGN, naamini hata baadhi ya Wanasimba wanaumiza vichwa kuhusu mchezo huu, ili kukisaidia kikosi chao kushinda siku hiyo kwa kuja uwanjani kwa wingi April 03.” Amesema Ahmed Ally

Tayari Simba SC imeshaanza kuuza tiketi za mchezo huo utakaopigwa saa moja usiku, huku Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ likitoa kibali cha mashabiki 35,000 wataoshuhudia mchezo huo wakiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kabla ya mchezo huo wa mwisho, Msimamo wa ‘Kundi D’ unaonyesha ASEC Mimosas inaongoza ikiwa na alama 09, ikifuatiwa na RS Berkane yenye alama 07 sawa na Simba SC huku USGN ikishika nafasi ya nne ikiwa na alama 05.

Kabangu: Majaji, Mwamuzi mkatende haki
LIVE: Uzindua, Ukaguzi wa kiwanda cha Samani Msalato