Klabu ya Simba SC imethibitisha kuwa kwenye mpango wa kumpa barua ya kumuachia (Release Latter) Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrsion, ambaye usiku wa kuamkia leo alitambulishwa rasmi kuwa mchezaji halali wa Young Africans.
Kiungo huyo aliwahi kuutaka Uongozi wa Simba SC kumwandikia barua hiyo kwa msingi ya kutambulika kama mchezjai huru, kufuatia mkataba wake na klabu hiyo kufikia kikomo baada ya msimu wa 2021/22.
Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema Morrison atakabidhiwa barua yake wakati wowote kuanzia sasa, na amewataka wadau wa soka kufahamu kuwa, Klabu hiyo haifanyi hivyo baada muhusika kuzungumza na vyombo vya habari na kutoa maneno ya kuwatishia.
Amesema Simba SC haina tatizo lolote na Morrison, na wameamua kutangaza kuwa kwenye mpango wa kumpatia barua ya mumuachia kiungo huyo kwa moyo mweupe.
“Hatuna tatizo na Morrison, Release Letter yake tutampatia Kwa moyo mweupe kabisa na hii sio kwa sababu ametupiga mkwara Majuzi ila ni Kwa manufaa yake kisoka”
“Tumepata taarifa amesajiliwa na Young Africans na hii kwetu ni furaha kwa sababu ukiona Timu kubwa Simba inatema wachezaji halafu Timu ndogo zinamgombania kwa sababu kwenye Timu kubwa amekosa nafasi akacheze kwenye Timu ndogo hivyo ni jambo la heshima mno kwetu” amesema Ahmed Ally
Morrison amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Young Africans ambayo aliwahi kuitumikia kabla ya kutimkia Simba SC mwanzoni mwa msimu wa 2020/21.