Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC umetoa pole kwa aliyewahi kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Hassan Dalali kufuatia ajali aliyoipata juzi Jumatatu (Machi 07) jijini Dar es salaam.

Dalali alianguka na Bodaboda aneo la Rangi Tatu njia ya kuingilia Chamanzi, polisi ndio waliomtambua baada ya kumfikisha kituoni, na baadae alikimbizwa Hospitali ya Mbagala Zakiem .

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally ametoa pole na kumuombea kheri Kiongozi huyo wa zamani alipozungumza na Wasafi Media mapema leo Jumatano (Machi 09).

Ahmed amesema walishutushwa na taarifa za ajali iliyomkuta Hassan Dalali, na wamekua bega kwa bega na familia ya mzee huyo ambaye bado ana mapenzi ya dhati ya klabu ya Simba SC.

“Tupo pamoja na familia ya Mzee Dalali katika kipindi hiki ambacho ni kigumu kwake, tunaamini Mungu atamuwezesha kuwa na afya njema na kurejea katika majukumu yake.” amesema Ahmed Ally.

Mzee Dalali, alipata ajali ya kuangushwa na Bodaboda kwenye korongo, akitokea Uwanja wa Benjamin Mkapa, kushuhudia timu yake ikicheza dhidi ya Dodoma Jiji, Juzi Jumatatu (Machi 09).

Biden apiga marufuku uagizaji wa mafuta Urusi
Serikali kuifumua sheria ya ndoa