Klabu ya Simba SC imeiomba Bodi ya Ligi Tanzania Bara ‘TPLB’ kuahirisha mchezo wa Mzunguuko watano wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Big Stars, ili kupata muda wa kujiandaa na mchezo wa Africans Football League dhidi ya Al Ahly.

Simba SC inatakiwa kucheza dhidi ya Singida Fountain Gate Jumapili (Oktoba 08) katika Uwanja wa Liti mjini Singida, baada ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa keshokutwa Alhamis mjini Mbeya katika Uwanja wa Sokoine.

Mapema leo Jumanne (Oktoba 03) Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC Imani Kajula amethibitisha kuwasilisha ombi hilo ‘TPLB’ ili kuuondoa mchezo huo na kuupangia tarehe nyingine.

Amesema kusudio kubwa la kuwasilisha ombo hilo ‘TPLB’ ni kutaka kutoa nafasi kwa wachezaji wao kupumzike na kisha kujiandaa na mchezo wa African Football League dhidi ya Al-Ahly utakaopigwa Oktoba 20, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

“Tuna imani na benchi letu la ufundi, tuwape muda watafanyia marekebisho kuhusu maoni ya mashabiki na wanachama”

“Tuna ratiba ngumu sana, tutacheza na Tanzania Prisons October 5 ugenini, kisha Singida fountain gate ugenini October 8 halafu Al Ahly October 20.”

“Tungeomba bodi ya ligi ituondolee mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate, ili tuweze kujiandaa vizuri na wachezaji wapumzike kwa sababu wametoka kwenye mechi ngumu.” Amesema Imani Kajula

Kalvin Phillips kumbadili Partey
Victor Osimhen avunja ukimya SSC Napoli