Mabingwa wa soka Tanznaia bara Simba SC wataanzia ugenini katika harakati za kusaka ubingwa wa Afrika, dhidi ya Plateau United ya nchini Nigeria kati ya Novemba 27-29 na watarudiana jijini Dar kati ya Desemba kati ya 4-6.

Hiyo imefahamika baada ya Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kupanga ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani humo jana Jumatatu Novemba 09 mjini Cairo, Misri.

Endapo Simba SC itafaulu mtihani wa kushinda michezo yake dhidi ya Plateau United iliyopewa namba 39, 40, itavaana na mshindi wa mchezo namba 37, 38 itakazokutanisha timu za CD do Sol ya Msumbiji dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.

Wakati Simba ikipangwa kuanzia nchini Nigeria, Namungo FC  wamepangwa kuvaana na Al Rabita ya Sudan Kusini wakianzia nyumbani Tanzania katika mchezo wa mkondo wa kwanza.

Namungo ilipata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kushika nafasi ya pili kwenye michuano ya ndani (ASFC).

Endapo Namungo FC watafanikiwa kushinda michezo yote miwili dhidi ya Ligi Kuu ya Al Rabita ya Sudan Kusini watacheza dhidi ya El Hilal Obeid ya Sudan.

Wakati huo huo Mabingwa wa soka visiwani Zanzibar Mlandege FC wamepangwa kukutana na CS Sfaxien ya Tunisia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku KVZ FC wakipewa El Amal ya Sudan, kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho.

Kaze awashukuru mashabiki, aisukia mipango Namungo FC
Trump amtumbua Waziri wa Ulinzi