Uongozi wa Simba SC umethibitisha kupokea taarifa kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ inayotoa nafasi ya kuingiza Mashabiki 35,000 Uwanja wa Benjamin Mkapa wakati wa mchezo wa Mzunguuko wa 04 wa Kundi D, Kombe la Shirikisho dhidi ya RS Berkane ya Morocco.
Simba SC itakua mwenyeji wa mchezo huo, utakaopigwa Jumapili (Machi 13), huku ikiwa na deni la kulipa kisasi cha kufungwa mabao 2-0, kwenye mchezo wa Mzunguuko wa 03 wa Kundi D, uliounguruma mjini Berkane-Morocco Februari 27.
Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amezungumza na WASAFI MEDIA mapema leo Jumatano (Macho 09), na kuthibitisha taarifa za kuruhusiwa kwa mashabiki 35,000, idadi ambayo ni sawa na ile ya mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza dhidi ya ASEC Mimosas uliomalizika kwa Mnyama kuchomoza na ushindi wa mabao 3-1.
“Tulitamani kupata ruhusa ya kuwa na mashabiki wengi zaidi uwanjani wakati wa mchezo wetu dhidi ya RS Berkane, lakini taarifa ya CAF imesisitiza lazima tuwe na mashabiki 35,000.”
“Tuliwaombwa CAF kuwa na mashabiki 60,000, lakini wameturuhusu kuwa na idadi hiyo 35000 ya mashabiki, hivyo tunawahimiza mashabiki wetu kufiwa Uwanjani ili kuzitendea haki nafasi hizo tulizozipata.” amesema Ahmed Ally.
Simba SC itakua na kazi kubwa ya kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya RS Berkane ili kujitengenezea njia nzuri ya kufuzu hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho, huku wageni wao kutoka Morocco wakiwa na lengo kama hilo.
Hadi sasa Msimamo wa Kundi D, unaonyesha kuwa RS Berkane inaongoza ikiwa na alama 06, ikifuatiwa na Simba SC yenye alama o4 sawa na USGN ya Niger huku ASEC Mimosas ya Ivory Coast ikiburuza mkia ikiwa na alama 03.